Kampuni iliyojengwa kuzunguka mchakato wa usajili wa Tanzania
Elimika Ung'are Professional Service Firm ni kampuni inayoongoza katika ushauri na huduma za kibiashara, iliyobobea katika huduma mbalimbali zikiwemo: Masuala ya Kampuni na Udhibiti, Kodi na Huduma za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), Uhasibu na Utoaji Taarifa za Fedha, Huduma Maalum za Fedha na Ufadhili, Bidhaa na Suluhisho za TEHAMA, Ukaguzi na Uhakiki (Audit & Assurance), Huduma za Kimkakati za Mtandaoni, Usimamizi wa Rasilimali Watu, Uuzaji na Uwekaji Chapa, Usimamizi wa Mnyororo wa Ugavi, Huduma za Kisheria na Usafirishaji, Usimamizi wa Ofisi ya Nyuma, Mafunzo ya Kitaalamu yenye Ujuzi Maalum, pamoja na Ushauri Kamili wa Kibiashara.
Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu
Mpoki A. Mwaiswaswa
Mwanzilishi na Mtendaji Mkuu (Founder & CEO)
+255 766 656 758 +255 655 056 758 Wasiliana kwa WhatsAppZaidi ya usajili: tunajenga uwezo wa biashara yako
Elimika Ung'are Professional Service Firm vilevile tunaandaa programu maalumu za elimu na mafunzo ya biashara pamoja na ushauri kwa wafanyabishara na wajasiriamali wadogo (Business Consultations Services) ili kuongeza ufanisi katika maeneo mbalimbali muhimu ya biashara. Lengo letu ni kuhakikisha Watanzania wengi wanapata elimu, mafunzo na ushauri juu ya biashara, ujasiriamali, uwekezaji na fursa mbalimbali za kiuchumi na maendeleo nchini Tanzania.
Sisi Elimika Ung'are Professional Service Firm tunaunganisha ujuzi, maarifa, umahiri na weledi kwenye kutoa elimu, mafunzo na ushauri katika mwaswala ya usimamizi na menejimenti ya biashara, usimamizi wa fedha, usimamizi na uchambuzi wa sera na sheria za biashara nchini, mauzo na masoko, uwekezaji pamoja na ushauri katika mifumo ya TEHAMA katika biashara nchini Tanzania.
Huduma zetu zinazingatia ufanisi, uharaka, wepesi, uaminifu, weledi na ubora wakati wote wa kazi. Elimika Ung'are Professional Service Firm ina washauri na watalamu wa uchumi, biashara na uwekezaji wenye ujuzi wa kufanya upembuzi yakinifu na makini katika masuala ya uwekezaji, biashara na ujasiriamali nchini Tanzania.
Makundi manne ya watu wanaolengwa kunufaika na huduma zetu
-
1
Watu wenye mawazo ya biashara
Katika jamii yetu wapo watu ambao wanayo mawazo ya kibiashara au nia ya kuanzisha shughuli ya uzalishaji lakini wanakosa maarifa sahihi ya namna gani ya kisheria kuyaweka mawazo yao kimatendo. Wengi wakisikia mchakato wa kisheria unaohitajika ili biashara zao ziwe halali wanakata tamaa. Ikiwa wewe ni mmojawapo una wazo lakini hujui ni mfumo upi utakufaa kuendesha wazo lako kisheria basi ni muhimu sana kuonana na watalamu wetu ama kutufuatilia katika kurasa zetu mitandaoni kwani tunaendelea kutoa maarifa yanayoweza kukusaidia namna bora ya kutekeleza wazo lako kwa mujibu wa sheria.
-
2
Watu wenye biashara au shughuli ambayo haijarasimishwa
Eneo hili lina watu wengi sana wanaoendesha shughuli au biashara zao pasipo kuwa na usajili au kurasimishwa na mamlaka mbalimbali. Hapa tunazungumzia mifano mingi ya shughuli au huduma kama za wamachinga, wafanyabiashara wa masoko, mama lishe, wafanyabiashara maeneo ya standi za magari n.k. kwa kiasi kikubwa uchumi wa wanachi unazunguka kwa aina ya watu ambao wanaendesha shughuli zao katika mfumo usio rasmi. Ikiwa wewe ni mmoja wapo ya watu wanaoendesha shughuli au biashara katika mfumo usio rasmi, basi swala la kuhudumiwa na sisi Elimika Ung'are Professional Service Firm linakuhusu sana kwani utajifunza faida na namna mbalimbali zinazoweza kukusaidia biashara au huduma yako kukua endapo utaifanya kuwa rasmi na kutambulika na mamlaka husika.
-
3
Watu wenye mtaji wenye nia ya kuendesha biashara
Wapo watu ambao wana vipato au mitaji mikubwa ya kuweza kuwekeza katika biashara au huduma za uzalishaji lakini hawana maarifa ya namna bora ya kuwekeza mitaji yao. Katika huduma zetu za ushauri wa uwekezaji utajifunza namna nzuri za kisheria zinazoweza kukusaidia kuchukua hatua nzuri za uwekezaji wa mtaji wako kwenye huduma au biashara na kukupatia faida nzuri kwa matumizi ya baadaye. Tutaeleza njia nzuri za kuanzisha biashara binafsi au za ushirika baina yako na watu wengine kwa lengo la kufikia faida nzuri ya pamoja.
-
4
Waajiriwa wenye nia ya kuwa na biashara/shughuli nyingine ya kuingiza kipato
Hapa tunagusa kundi kubwa la watu walioajiriwa na wana kiu na matamanio ya kuwa na biashara zao au huduma wanazotaka kutoa kwa jamii. Changamoto kubwa wanayoyoiona ni ukosefu wa muda na usimamizi bora wa huduma au biashara wanazokusudia kufanya.
Tunachofanya
Tunaongoza biashara katika kila hatua ya urasimishaji: kusajili jina la biashara, kampuni ya ndani au kampuni ya kigeni na BRELA; kupata TIN na kuweka mifumo ya TRA na EFD; kujiandikisha na NSSF; na kupata leseni sahihi ya Schedule A au Schedule B. Zaidi ya usajili, tunatoa ushauri endelevu kuhusu masuala ya kampuni, kodi, uhasibu, ufadhili na uendeshaji wa ofisi ya nyuma.
Wamiliki wengi wa biashara Tanzania wanafanya kazi bila kusajiliwa rasmi, jambo linalowazuia kupata mikopo, huduma za maendeleo ya biashara, na mikataba na kampuni kubwa za ndani na za kigeni. Tupo hapa kuziba pengo hilo, na kuhakikisha biashara zinaendelea kuzingatia sheria baada ya kuwa rasmi.
Kwa nini utuchague
- Ujuzi wa sheria za ndani. Ujuzi wa kisasa na wa vitendo kuhusu matakwa ya BRELA, TRA na NSSF, unaosasishwa kadri sheria zinavyobadilika.
- Kampuni moja, hatua zote. Usajili, kodi na leseni vinashughulikiwa pamoja, hivyo jukumu halisambazwi kati ya washauri tofauti.
- Ufuatiliaji wa tarehe za mwisho. Tunafuatilia tarehe za uhuishaji wa leseni na uwasilishaji wa nyaraka kwa niaba yako, ili adhabu zisijilimbikize bila kujua.
- Huduma kwa nchi nzima. Tuko Mbeya na tunahudumia wateja kote Tanzania, tukiwa na msaada wa usajili wa mbali popote ulipo.
Sekta tulizowahi kusajili
Fanya kazi na kampuni inayoendelea kukusaidia baada ya usajili.
Wasiliana nasi kuzungumzia biashara yako.
Wasiliana nasi